Askari wa kike, Hannan Halfani anagundua siri kubwa ya kupangwa kwa mpango wa kumuua rais Mark Mwazilindi akiwa katika maliwato ya ikulu. Kutoka katika mdomo wa Hannan, anaisafirisha siri hiyo hadi katika sikio la mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba. Daniel na Hanna wakishirikiana na mpelelezi wa kujitegemea, Martin Hisia, wanaingia kazini na kuanza kuchunguza kisa cha kupangwa kwa kifo cha rais. Unakuwa ni uchung uzi mgumu sana. Uchunguzi unaowa-pitisha katika msitu mnene na unaowapitisha katika matukio ya kutisha isivyo kawaida. Uchunguzi unaowafanya wawe karibu na kifo kuliko wakati wowote katika maisha yao ya kipelelezi. Kwa hakika, kunakuwa na mstari mwembamba sana kati ya maisha yao na kifo Bila kujua, kumbe walikuwa wameingia katika anga hatari sana za wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya nchini Tanzania. Madawa ambayo kwa sasa yamekuwa ni KIRUSI KIPYA. Wafanyabiashara hawa wanapanga kumuua rais Mark kwa kuwa amekuwa ni kikwazo kikubwa sana katika biashara zao. Wakina Daniel wanajikuta na kazi kuu mbili ngumu sana kuliko zote walizowahi kuzifanya, ya kwanza ni kuzuia kuawa kwa rais, ya pili ni kuwatia mbaroni watanvabiashara wote wa madawa havo haramu. Je wakina mpelelezi Daniel Mwaseba na wenzake watafanikiwa?