Sinaubi (Paperback)
 
作者: Mbwana Kidato 
書城編號: 26918284


售價: $289.00

購買後立即進貨, 約需 18-25 天

 
 
出版社: African Books Collective
出版日期: 2023/06/30
重量: 0.34 kg
ISBN: 9789987753734

商品簡介


Hii ni Riwaya ya kwanza ya Mbwana Kidato ambayo inatokana na tukio la kweli alilolisoma alipokuwa akipitia majarida mbali mbali ya Tanzania kwenye mtandao. Kwenye kurasa za mbele, alikutana na habari ya kuhuzunisha. Ilikuwa ni habari ya msichana mwenye ulemavu wa ngozi aliyekatwa viungo vya mwili wake. Hii ni kazi ya mwandishi, kazi ya kufikirika, yenye kuelimisha, kuakisi maisha yetu na kutuuliza maswali juu ya utu wetu. Je miongoni mwetu kuna wengine wana utu wenye thamani zaidi ya utu wa wengine? Kama kuna kipimo cha utu, huo utu unapimwa na kipimo cha aina gani? Je kipimo hicho ni maumbile yetu au ni tabia zetu? ama ni vitu vinavyo tuzunguka? Muandishi anajaribu kuuliza haya maswali, kupitia muhusika mkuu wa riwaya hii ambaye ni 'SINAUBI'.


Mbwana Kidato ni mtengenezaji wa vipindi vya runinga na filamu. Amepata elimu yake nchini Uingereza kwenye nyanja za uandaaji, utengenezaji, uandishi na uhariri wa picha za vipindi vya filamu na runinga. Ameshawahi kufanya kazi na Shirika la Utangazaji la Tanzania, kama mtayarishaji wa vipindi. Siyo mara yake ya kwanza kuandika, (film scripts) lakini kazi yake imekuwa ikilenga zaidi hadhara ya upande wa runinga. Safari hii ameandika riwaya/tamthilia kwa hadhara yote, yaani hadhara ya wasomaji vitabu na hadhara ya waangaliaji runinga na filamu.

* 以上資料僅供參考之用, 香港書城並不保證以上資料的準確性及完整性。
* 如送貨地址在香港以外, 當書籍/產品入口時, 顧客須自行繳付入口關稅和其他入口銷售稅項。

 

 

 

  我的賬戶 |  購物車 |  出版社 |  團購優惠
加入供應商 |  廣告刊登 |  公司簡介 |  條款及細則
 
  香港書城 版權所有 私隱政策聲明
 
  顯示模式: 電腦版 (改為: 手機版)